Endelea Kuisikiliza Redio Ihsaan Fm

Endelea Kuisikiliza Redio Ihsaan Fm

Tuesday, December 3, 2013

News

Ngome ya Jeshi yapigwa Nigeria
Wapiganaji wa Boko Haram wameshambulia ngome ya kikosi cha anga cha Jeshi Kaskazini Mashariki mwa Nigeria na kuharibu helkopta mbili maafisa wa serikali wamesema.

Mashuhuda wa tukio hilo wamesema kuwa mamia ya wapiganaji wameshambulia maeneo kadhaa katika mji wa Maiduguri kuanzia mapema asubuhi siku ya jana jumatatu.
Amri ya kutotembea ovyo ya saa 24 imetangazwa katika jimbo la Maiduguri. Na uwanja wa ndege unaotumiwa na wananchi umefungwa kwa muda.
Kwa mujibu wa taarifa  toak huko zinadai kuwa shambulio hilo ni shambulio kubwa ambalo limerudisha nyuma juhudi za Jeshi la Nigeria.
Tangu mwaka 2009 kikundi cha wapiganaji cha  Boko Haram walianza  mashambulizi ya kutaka kusimika utawala  utakaotumia sheria za kiislamu.

Mfuko wa China Na Afrika Kuongeza uwekezaji Afrika.
Mfuko wa maendeleo wa China na Afrika ambao unajulikana kama CADFund, utaongeza uwekezaji barani Afrika kwenye maeneo ya utegenezaji, miundo mbinu, kilimo na mengineyo.
Akizungumza kwenye mkutano wa masoko yenye ongezeko kubwa barani Afrika uliofunguliwa jana mjini Addis Ababa, naibu mkurugenzi wa CADFund Wang Yong amesema ongezeko la kasi la watu wenye mapato ya kati limeshuhudiwa barani Afrika, hali ambayo italeta ongezeko la kasi la mahitaji sokoni, ndiyo maana mfuko huo umeamua kuongeza uwekezaji katika utengenezaji ili kukidhi mahitaji ya wenyeji na kupunguza matumizi ya fedha za kigeni katika kununua bidhaa kutoka nje ya nchi.
Ameongeza kuwa miundo mbinu, kilimo na maeneo ya viwanda ni nyanja zinazofaa zaidi kufanyiwa ushirikiano kati ya China na Afrika, kwa kuwa nyanja hizo zinaweza kuimarisha uwezo wa kiuchumi wa Afrika na kuleta faida kwa mfuko huo.
Mpaka sasa mfuko huo umewekeza vitega uchumi kwenye miradi zaidi ya 72 iliyoko katika nchi 30 barani Afrika.

Waziri Mkuu Somalia awashutumu Wabunge
Baada ya wabunge wa nchi ya Somalia kupiga kura ya kutokua na imanai na Waziri mkuu wake,Waziri huyo Abdi Farah Shirdon amesikitishwa na hatua ya wabunge wa Somalia kupiga kura ya kutokuwa na imani naye na kuwatuhumu wabunge kwa kutompa nafasi ya kujitetea.
Abdi Farah Shirdon,ambaye amekuwa waziri mkuu wa Somalia kwa zaidi ya mwaka amejikuta akipoteza nafasi yake baada ya kupigiwa kura ya kutokuwa na imani naye baada ya kukataa shinikizo la kujiuzulu kutoka kwa raisi wa taifa hilo Hassan Sheikh Mohamud.Spika wa bunge la somalia Mohamed Osman Jawari, alibainisha kura 184 kati ya 249 za wabunge waliopiga kura walipiga kura ya kutokuwa na imani naye.
Aidha Spika Jawari ameongeza kuwa waziri mkuu huyo na serikali yake ataendelea na majukumu yake hadi atakapoteuliwa waziri mkuu mwingine.Wabunge wa Somalia walipiga kura ya kukosa imani na Waziri Mkuu Abdi Farah Shirdon, kwa tuhuma za ufisadi na kusabisha mgogoro ndani ya serikali aliyoiunda mwaka mmoja uliopita.

Iran kushiriki mazungumzo kuhusu amani ya Syria
Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nchi za Nje ya Marekani Jane Sake amesema kuwa hadi sasa bado haujachukuliwa uamuzi wa kualikwa au kutoalikwa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran kwenye kikao cha Geneva 2 kitakachojadili amani ya Syria.
Sake amesema kuwa, wawakilishi kutoka Marekani, Russia na Umoja wa Mataifa watakutana tena tarehe 20 Disemba kwa lengo la kujadili jinsi ya kuandaliwa kikao hicho kitakachojadili kadhia ya Syria. Amesema kuwa, sharti la kushiriki Iran kwenye mazungumzo ya Geneva 2 ni kukubali taarifa iliyotolewa mwishoni mwa kikao cha Geneva1. Ameongeza kuwa, suala la ushiriki wa Iran litajadiliwa katika vikao vijavyo.
Inafaa kuashiria hapa kuwa, nchi za Magharibi zikiongozwa na Marekani, Uingereza na Ufaransa pamoja na washirika wao wa eneo la Mashariki ya Kati kama Saudi Arabia, Uturuki, utawala wa Kizayuni wa Israel  na Qatar zimekuwa mstari wa mbele kuwapatia misaada ya fedha na silaha wanamgambo wa makundi ya kigaidi nchini Syria kwa shabaha ya kuuangusha utawala wa Rais Bashar Assad uliochaguliwa na wananchi.